Home Music Diamond Platnumz Ft Tanzania All Stars – Lala Salama Magufuli

Diamond Platnumz Ft Tanzania All Stars – Lala Salama Magufuli [Mp3 Download]

3,395
Diamond Ft Tanzania All Stars – Lala Salama Magufuli
 • Diamond Platnumz Ft Christina Shusho , Jux , Mbosso , Joel Lwaga , Marioo , Zuchu , Darassa , Barnaba , Maua Sama , Ben Pol , Lava Lava , Khadija Kopa , Malkia Karen , Dulla Makabila , Queen Darleen , Baba Levo , G Nako , Cyrill Kamikaze , Mrisho Mpoto , Chege , Rayvanny , Madee , Belle 9, Maarifa & Abby Chams – Lala Salama Magufuli.

  Wasafi Media presents to you a brand new song tagged as a tribute song dedicated to the late and former president of The republic united of Tanzania John Pombe Magufuli.

  RELATED: Diamond Platnumz – Super Woman Ft Tanzanian Men All Star

  This song features all top Bongo Fleva and Hip Hop artists in Tanzania including; Diamond Platnumz Ft Christina Shusho , Jux , Mbosso , Joel Lwaga , Marioo , Zuchu , Darassa , Barnaba , Maua Sama , Ben Pol , Lava Lava , Khadija Kopa , Malkia Karen , Dulla Makabila , Queen Darleen , Baba Levo , G Nako , Cyrill Kamikaze , Mrisho Mpoto , Chege , Rayvanny , Madee , Belle 9, Maarifa & Abby Chams

  RELATED: Zuchu – Tanzania Ya Sasa (Prod. Lizer)

  Apart from being the president of Tanzania Late Magufuli served as Minister of Works, Transport and Communications from 2000 to 2005 and 2010 to 2015 and was chairman of the Southern African Development Community from 2019 to 2020.

  Similar songs dedicated to Late Magufuli

  Lyrics

  [Mbosso]

  Nalifuta chozi kushoto
  Kulia latiririka
  Maumivu moyo wa moto
  Nafsi yatatarika

  Vilio wakubwa watoto
  Iyoo we zinasikikika
  Wachonge zetu changamoto
  Wapi zitashikika

  [Christina Shusho]
  Umelala iyoo, baba umelala wee
  Nenda we Magufuli nenda wee
  Tulikupenda Mungu kakupenda zaidi
  Baba nenda wee, baba nenda wee

   

  [Jux]
  Yaani baba (Baba)
  Tutakukumbuka kwa mazuri yako
  Sema baba (Baba)
  Tutakukumbuka kwa upendo wako

  [Madee]
  Kuna Muda nalega nakosa power
  Nasema no God hii sio sawa
  Mbona kuna wengi tu walipaswa kwenda
  Unajibu “NO” huyu niliyempenda

  Umempenda John, umemchukua john
  Umetuacha hatuoni sio alfajiri sio jioni
  Tukifikicha mboni kule mbele hatuoni
  Mungu akulaze baba mahali pema peponi

  [Joel Lwaga & Diamond Platnumz]
  Kweli vyema havidumu
  Ni machozi na uchungu
  Ni ghafla, ni ghafla
  Asante kwa kujenga Tanzania imara
  Nenda, nenda, nenda ulale

  Ulale salama, pumzika baba
  Ulale salama, kazi umeifanya
  Ulale salama, tutakuenzi daima
  Ulale salama

  [Zuchu]
  Huzuni imetawala
  Jembe Tanzania limetutoka
  Yaani kama masihara leo taifa tunahuzunika
  Baba uende salama, tutakukumbuka sana
  Akupake Maaulana Amina

  []
  Miundo mbinu tunaona (Ona)
  Elimu bure tunasoma (Soma)
  Makao makuu kwetu Dodoma
  Umetupa heshima baba

  [Khadija Kopa]
  Eti njia yetu ni moja
  Umetanguli si tunafuatia
  Tunajikongoja taifa laumia
  Tunakulilia

  [Baba Levo]
  Kiumbe jasiri tena mahiri
  Ametutoka (Ametutuka)
  Jasiri mwenye akili
  Ametutoka (Ametutoka)
  Magufuli wewe ameondoka
  Simanzi Tanzania ametutoka

  [Mrisho Mpoto]
  Ina maana mapambano kikomo ndio imefikia
  Vuta nikuvute historia inakwenda kubakia
  Kila ulimi kifafa umeshikwa
  Hauwezi kusema hauwezi kuteta
  Daima ulisema tukuombee
  Ah, ila mauti yamevikwa taji dhidi ya dua
  Daima tutakukumbuka

  [Rayvanny]
  Jioni jua limezama
  Umetangulia ulale salama
  Kila ulosema limetimia
  Serikali Dodoma imehamia
  Baba mbona hujasubiria
  Ikulu ulojenga mwenyewe hujaingia

  Ulale, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama
  Ula ula ulale, ulale salama
  Ulale salama (Ulale baba)

  Lala, lala
  Lala lala
  Lala lala

  [G Nako]
  Kilio ukiskie kwa jirani
  Machozi machozi nani afute nani?
  Kifo kifo, kifo kifo
  Kifo fumbo kubwa duniani

  [Lava Lava]
  Ni mengi ulituhusia
  Upendo mimi na yule
  Elimu bora ukatupatia
  Watoto waende shule

  Tuchape kazi ukasisitizia
  Tusikae bure
  Mbona sasa umetukimbia
  Umetuacha na simanzi baba

  [Darassa]
  Mungu ana njia zake huwezi hata kumuotea
  Mungu anachukua hata unachokinyenyekea
  Unachotegemea nguzo yako kuegemea
  Ndio maana dini zinasema tuishi kwa ku prepare

  Look alas, now we breathe like there is no air
  Should I continue singing?
  Or let me pray for better days to come
  Rest in Peace uncle Magu till we meet again Amen

  []
  Umetutoa kwenye sifuri mpaka uchumi wa kati
  Madaraja babara nzuri ona mwendo kasi

  [Khadija Kopa]
  Wanawake umetusimamia
  Kwenye sekta mbalimbali
  Umetusimamisha umetuinua

  Ulivyomteua Samia
  Umetupa ujasiri tupambane
  Asante Magufuli

  []
  Kila saa uliimaliza migogoro
  Njoo uuzindue mradi wako Morogoro
  Baba (Baba) Baba (Baba)

  Hivi sivyo tulivyotegemea
  Imeanguka nguzo tuloegemea
  Baba (Baba) Baba (Baba)

  Ulale Salama
  Ulale salama, ulale salama
  Asante kwa wema wako
  Ulale salama, asante kwa wema wako
  Ulale salama

  [Queen Darleen]
  Matibabu bure kwa watoto na wazee
  Hukutuacha nyuma wanawake twendelee

  [Marioo]
  Atufute nani machozi
  Taifa lakulilia
  Atatuvusha nani mwokozi
  Na nahodha umetangulia

  Yametutawala majonzi
  Baba umetukimbia
  Zimetushafura pozi
  Huzuni imetuelemea baba

  [Abby Chams]
  Nuru yaangaza taifa
  Imekatizwa ghafla
  Magufuli baba yetu
  Tutakukumbuka daima

  Pumzika kwa amani
  Is out of faith —
  All have left is memories
  And — let go

  []
  Hukuwa Mungu tujue umetimia
  Singeshindwa ubaki wewe
  Ili achukue vichaa mia
  Ila kama ambavyo mwewe hachagui kuku
  Maiti hachagui sanda na kifo hakichagui mtu

  [Barnaba Classic]
  Kina mama wenye hali za chini
  Bodaboda hali za chini
  Raia hali za chini
  Wanakuita Magufuli simama

  Najihisi kukata tamaa
  Ila inanibidi nikubali
  Ila Magufuli simama

  Ni mengi uliyotenda kwa ushujaa
  Haitoshi ulikuwa mzalendo
  Magufuli simama
  Uliipigania haki hukubagua watu wala mtu
  Magufuli simama

  []
  Mkombozi wa wanyonge umeenda (Aah umeenda)
  Jasiri mtenda haki umeenda (Aah umeenda)
  Kipenzi cha wananchi umeenda (Aah umeenda)
  Mpenda maendeleo umeenda (Aah)

  [Chege]
  Baba ulale salama, ulale salama
  Daddy ulale salama, ulale salama
  Hivi kweli tutacheza tena, ulale salama, ulale salama
  Uuu la, ulale salama, ulale salama

  [Cyril Kamikaze]
  Kiongozi jasiri ambaye alipinga rushwa
  Alinyanyua wanyonge pale tu alipoangushwa
  Hakuogopa fisadi yeyote yeye alimgusa
  Huduma kwa wakati bila hata kuzungushwa
  Ona barabara vijijini tunafika
  Pumzika peponi chuma daima utakumbukwa
  Ulale salama, uuuuu..

  [Diamond Platnumz & Tanzania All Stars]
  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama

  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama
  Ulale salama, ulale salama