Sarah Amuomboleza Cohen kwa Usemi wenye Majonzi

Sarah Amuomboleza Cohen kwa Usemi wenye Majonzi

305

Sarah Wairimu's moving tribute during late husband Tob Cohen's burial

Marehemu Tob Cohenhatimaye alizikwa kwenye Makaburi ya Wayahudi jijini Nairobi. Kati ya waliokuwepo katika mazishi hayo ya mfanyabiashara huyo alikuwa ni mkewe, Sarah Wairimu, ambaye pia ni mtuhumiwa mkuu katika mauaji yake.

Akihudhuria mazishi hayo chini ya ulinzi mkali, Wairimu alitoa usemi mzito na kumuomboleza bwanake Cohen .

“Kifo cha Cohen kimekuwa kikiniumiza sana. Kifo kimeninyang’anya mtu jasiri na mpendwa.”

Sarah Wairimu's moving tribute during late husband Tob Cohen's burial

Alimuomba mungu kuhakikisha kuwa haki ilitendeka na wahalifu hao wamepatikana.Pia, alisema kuwa amewasamehe wale ambao wameamua kumhukumu vibaya.

Mwili wa Cohen ulihamishwa kutoka kwa eneo la kuhifadhia maiti la Chiromo hadi kaburi la Wayahudi kwenye barabara ya Wangari Maathai kwa ibada za mwisho. Baadhi ya watu maarufu mazishi hayo kuhudhuria ni pamoja na balozi wa Uholanzi na binamu za Rais Uhuru Kenyatta, Kapteni Kung’u Muigai na Ngengi.

Hata hivyo, dadake Cohen hakuhudhuria mazishi hayo. Hii ni baada ya yeye kurudi uholanzi siku moja baada ya Urathi wa Cohen kusomwa.

Mwili wa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 72 ulipatokan umetukwa kwenye tangi la maji chini lilokuwa ndani ya ua nyumbani kwake.

Source link