Rafiki wa De Mathew, Kamande Wa Kioi apata ajali mbaya

Rafiki wa De Mathew, Kamande Wa Kioi apata ajali mbaya

318

Msanii wa Benga wa Kikuyu Kamande Wa Kioi alipata ajali ya barabara kwenye eneo la Githurai siku ya Alhamisi.

Ripoti ilisema kuwa gari la Kioi liligongana ana kwa ana na basi ya Nazigi Sacco kwenye barabara ya Kamiti.

Msanii huyo alikimbizwa kwa hospitali na wasamaria wema ambao walishuhudia ajali hiyo.

Picha zilizopatikana zilionyesha jinsi gari hilo liligongwa kupindukia.

Tulijaribu kumpata msanii huyo kwa simu wakati wa kuandika jarida hili lakini maombo yetu hayakufua dafu. Walakini, chanzo alielezea kuwa msanii hakuhitaji matibabu wa kina kwani alipata majeraha madogo.

Kioi anafahamika sana kwa nyimbo kama vile  Funny, Uhuru ni Witu (Uhuru ni wetu), Karanga Chapo, Mu-Ovacado na Marigiti.

Hii ilikuwa ajali ya pili kuhusisha wasanii wa benga baada ya kifo cha rafiki yake marehemu De Mathew.

De Mathew mwezi wa Agosti alipata ajali mbaya wa barabara na akafariki alipogonga lori kando ya hoteli ya Blue Post.

Source link